Posts

YAFAHAMU MAKOSA YASIYO NA DHAMANA

YAFAHAMU MAKOSA YASIYO NA DHAMANA Dhamana ni haki ya yako kikatiba, lakini Kuna makosa ukitenda hukuondolea haki hiyo na hivyo kunyimwa dhamana makosa hayo ni kama yafuatayo:- (i) mauaji, uhaini, ujambazi wa kutumia silaha, au unajisi wa mtoto. (ii) usafirishaji haramu wa madawa ya kulevya kinyume cha Sheria ya Madawa ya Kulevya na Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Madawa ya Kulevya, lakini haihusu mtu aliyeshitakiwa kwa kosa la kukutwa na madawa ambayo kwa kuzingatia mazingira yote ambako kosa lilitendeka, haikuwa kwa makusudi ya usafirishaji au kibiashara. (iii) kosa linalohusisha heroini,kokeini, opiamu iliyotayarishwa opiamu popi (papava setijeramu), majani ya popi, mmea wa koka, majani ya koka, kanibisi sativa au kanibisi resini (Heipu ya India), methakyolani (mandraksi), kata edulisi (khati) au dawa nyingine ya kulevya au kitu cha saikotropiki kilichooreshwa kwenye jedwali la Sheria hii ambayo ina thamani iliyothibitishwa na Kamishina wa Kamisheni ya Taifa ya Uratibu wa Uthib...